Matangazo ya moja kwa moja ya Bunge Maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Yatarushwa hapa pindi Bunge litakapokuwa kwenye Mjadala

Dodoma Tanzania, 2014

 • kakaMwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta akutana na uongozi wa Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) linaloongozwa na ndg Deus Kibambaleo Ofisini kwake Dodoma Wakati Bunge hilo likiendelea na vikao vyake kwa mujibu wa sheria
 • kakaMwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta akitoka nje ya ukumbi wa Bunge Maalum, akiongozwa na mpambe wa Bunge Maalum pamoja na makatibu mezani wa kikao cha siku hiyo, baada ya kumaliza shughuli za Bunge Maalumu zilizokuwa zimepangwa kufanyika kwa siku hiyo. Wa mwisho ni Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Maalum ndg. John Joel.
 • kakaMakamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Mhe. Samia Suluhu akifanya mahojiano na Watangazaji wa Bunge TV wakiongozwa na ndg. Allen Mbaga, kwa ajili ya kutoa Elimu kwa Umma kuhusu Bunge Maalum na vikao vyake linaloendelea mjini Dodoma kwa mujibu wa sheria.
 • kakaMwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta akutana na kundi la Wafugaji Tanzania likiongozwa na mlezi wao Mhe. John Shibuda(MB) na Mjumbe, Bungeni Dodoma kufuatia Bunge Maalum linaloendelea na vikao vyake, kwa ajili ya majadiliano ya mambo yao ambayo waliyaomba yaingizwe kwenye Rasimu ya pili ya Muungano lakini hayakujumuishwa.
 • kakaMwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta akiwa katika kikao na uongozi wa jukwaa la wahariri Tanzania ukiongozwa na Ndg. Absalom Kibanda Ofisini kwake Bungeni Dodoma. Huu ni mwendelezo wa Mwenyekiti wa Bunge hili la kihistoria kupokea makundi mbalimbali yenye kuwakilisha wananchi katika Nyanja mbalimbali ili kuweza kuwasilikiliza kama kiongozi na kufikisha mawazo ya kila kundi sehemu husika kwa hatua zingine
 • kakaMwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Mh.Samuel Sitta akutana na viongozi wa wakulima wa pamba wa nchi nzima, wakiomba Bunge liendelee na vikao vyake kwa kuwa lipo kwa Mujibu wa sheria ya Mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 na masuala yao yazingatiwe ndani ya katiba, likiwemo suala la kutambua haki zao ambazo kwenye Rasimu ya pili hazikutajwa.
 • kakaKundi la 201, likiwa katika baadhi ya vikao vyake Agosti ,2014, likiongwazwa na kiongozi wake Mhe. Dr. Francis Michael, kujadili mambo magumu yanayosumbua vichwa vyao kwa niaba ya wananchi wanaowawakilisha, ili kuhakikisha kunakuwepo na ushiriki mzuri wenye Tija kwa Wananchi wanaowawakilisha na Taifa zima kwa ujumla.
 • kakaM/Kiti wa Bunge Maalum Mhe Samuel John Samuel Sitta akutana na Masheikhe kutoka Tanzania bara na, visiwani wamsifu kwa kuliendesha Bunge kwa weledi mkubwa na ukomavu wa kidemokrasia, pamoja na mambo mengine wamemuomba aendeleze weledi wake ili Katiba bora na yenye kutatua matatizo/ kero za wananchi ipatikane. Kwa kuhitimisha kikao hicho wameomba dua na kuliombea bunge liendelea vizuri na shughuli zilizokusudiwa.
 • kakaMwenyekiti wa Bunge Maalumu Mhe. Samuel John Sitta na Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Samia Suluhu wakutana na wasanii wa tasnia mbalimbali za sanaa wakiongozwa na Simon Mwakifamba Rais wa waandaaji filamu na ndg. John Kitime, Mwenyekiti wa mtandao wa wanamziki wakiomba Bunge Maalum lizingatie mambo yao waliyoyatoa kwenye tume na hayakuwekwa ikiwa ni pamoja na kipengele cha Haki za Miliki Bunifu (Intellectual Property Rights) na kuomba Bunge la katiba liendelee na mijadala yake kwa sababu linazingatia maoni na
 • kakaMwenyekiti wa kamati Na3 Mhe. Dkt. Francis Kasabubu Michael na wajumbe wa kamati yake kwa pamoja wakisiliza jambo kwa umakini kutoka kwa wasanii wa tasnia mbalimbali wakiwasilisha hoja zao ambazo wamezifafanua moja hadi nyingine ikiwemo ile ya Haki za Miliki Bunifu (Intellectual Property Rights) na kuomba Bunge la katiba liendelee na mijadala yake kwa sababu linazingatia maoni na mahitaji ya watanzania wote wa makundi mbalimbali kuhakikisha haki za msingi za kila kundi zinazingatiwa.
 • kakaDkt. Hamisi Andrea Kigwangalla Mjumbe wa kamati namba 4 akiendesha kikao kwa niamba ya mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Christopher Olonyokie OleSendeka. Hapa kamati inawasikiliza Wasanii ambao wanatembelea kamati moja hadi nyingine kwa ajili ya kuwasilisha mambo yao ya msingi likiwemo la Haki za Miliki Bunifu (Intellectual Property Rights) na kuomba Bunge la katiba liendelee na mijadala yake kwa sababu linazingatia maoni na mahitaji ya watanzania wote wa makundi mbalimbali kuhakikisha haki za msingi za kila
 • kakaMhe. Mizengo Pinda waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. William Lukuvi Waziri wa Nchi Sera Uratibu na Bunge, na wajumbe wa kamati namba 1 wakiwasikiliza Wasanii ambao wanatembelea kamati moja hadi nyingine kwa ajili ya kuwasilisha mambo yao ya msingi likiwemo la Haki za Miliki Bunifu (Intellectual Property Rights) na kuomba Bunge la katiba liendelee na mijadala yake kwa sababu linazingatia maoni na mahitaji ya watanzania wote wa makundi mbalimbali kuhakikisha haki za msingi za kila kundi z
 • kakaMjumbe wa kamati namba 3, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa mchango wake wa mawazo wakati kundi la wasanii wa sanaa mbalimbali walipotembelea kamati yao kueleza mambo ya msingi wanayo ona yakiwekwa katika katiba yatawasaidia katika kazi zao
 • kakaWajumbe wa kamati namba 8, wakishiriki kikamilifu katika baadhi ya vikao vya kamati yao. Pichani ni Mhe. Abdulkarim Shah mjumbe kutoka Bunge la Jamhuri na wajumbe wa kutoka 201 akiwemo Askofu Donald Leo Mtetemela.
 • kakaMwanasiasa mkongwe na Mjumbe wa kamati namba 8 Mhe. Kingunge Ngombale Mwiru, akitafakari jambo juu ya mjadala uliopo mezani kujadili Rasimu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano katika kamati yake. Mhe. Kingunge Ngombale Mwiru ni miongoni mwa wajumbe waliowasilisha michango yao katika Bunge Maalum ili iweze kupitiwa na kujadiliwa na wajumbe wote kwa maslahi ya Taifa na watu wake kwa ujumla.
 • kakaMwenyekiti wa Bunge Maalumu Mhe. Samuel John Sitta na Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Samia Suluhu wakipokea nyaraka iliyoandaliwa na wasanii wa tasnia mbalimbali, anayewasilisha kwao kwa niaba ya wasanii ni Ndg. Simon Mwakifwamba, Rais wa Shirikisho la filamu nchini(TAFF).
 • kakaMjumbe wa kamati namba 8, Mhe. Reuben R. Matango akishiriki katika baadhi ya vikao vya kamati yao, wakati wasanii wakiomba mambo yao yazingatiwe katika katiba yeye anaomba mambo ya wakulima pia yawekwe katika katiba ikiwemo haki ya wakulima na wafugaji.
 • kakaSehemu ya wajumbe wa kamati namba 9, Wakishiriki katika kamati yao kujadili Rasimu ya pili ya katiba.
 • kakaSehemu ya wajumbe wa kamati namba 1, Wakishiriki katika kamati yao kujadili Rasimu ya pili ya katiba, hapa wapo pamoja na kundi la wasanii wa Tasnia mbalimbali kujadili mambo yahusuyo kazi za sanaa.
 • kakaMjumbe wa kamati namba 1, Mhe Hamisi Mnondwa akitoa mchango wake wa mawazo wakati kundi la wasanii wa tasnia mbalimbali walipotembelea kamati yao kueleza mambo ya msingi wanayo ona yakiwekwa katika katiba yatawasaidia katika kazi zao, pembeni yake wanaomsikiliza ni Mhe. James Lembeli na Mjumbe mwingine wa 201.
 • kakaKwa hakika wasanii wamepokelewa na kusikilizwa hoja zao kama walivyosikilizwa makundi mengine ya Wafugaji na wavuvi, wakulima, wafanyakazi wanahabari n.k. Hapa viongozi na wajumbe wa Bunge maalum Mhe. Mizengo Pinda Waziri mkuu na Mhe. William Lukuvi waziri wa nchi sera uratibu na Bunge wakisikiliza hoja zinazowasilishwa na wasanii katika kamati yao namba 1.
 • kakaSehemu ya wajumbe wa kamati namba 9, Wakishiriki katika kamati yao kujadili Rasimu ya pili ya katiba, hapa wapo pamoja na kundi la wasanii wa Tasnia mbalimbali kujadili mambo yahusuyo kazi za sanaa.
 • kakaMwenyekiti wa Bunge Maalumu Mhe. Samuel John Sitta na Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Samia Suluhu wakimsikiliza Ndg. Simon Mwakifwamba, Rais wa Shirikisho la filamu nchini(TAFF) akiwasilisha mezani, pamoja na mambo mengine wameomba Bunge Maalum lizingatie mambo ya wasanii kama vile Haki za Miliki Bunifu (Intellectual Property Rights) na kuomba Bunge la katiba liendelee na mijadala yake, kwa sababu linazingatia maoni na mahitaji ya watanzania wote wa makundi mbalimbali kuhakikisha haki za msingi za kila kundi
 • kakaMwenyekiti wa kamati namba 1 Mhe Ummy Mwalimu, Makamu Mwenyekiti Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa na katibu wa kamati hiyo wakifurahi jambo wakati mjumbe wa kamati yao pichani hayupo akitoa mchango wake mbele ya kamati hiyo.
 • kakaMjumbe wa kamati namba 1 katika Bunge Maalum ambaye pia ni waziri wa ulinzi, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi na pembeni yake Ndg. Simon Mwakifwamba, Rais wa Shirikisho la filamu nchini(TAFF)
 • kakaNdg. Simon Mwakifwamba ambaye ni Rais wa Shirikisho la filamu nchini(TAFF) akitambulisha msafara wake kwa wajumbe wa kamati namba 9 meza kuu ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Kidawa Salehe na Makamu Mwenyekiti Mhe. William Ngeleja pamoja na makatibu wa kamati hiyo.
 • kakaMwenyekiti wa kamati namba 9 Mhe. Kidawa Salehe na Makamu Mwenyekiti Mhe. William Ngeleja wakipokea mezani hoja zilizowaslishwa kwao na ndg. John Kitime ambaye ni mwenyekiti wa mtandao wa wanamziki nchini kwa niamba ya wasanii wa Tasnia mbalimbali. Wanaochukua muhtasari ni makatibu wa kamati hiyo.
 • kakaMjumbe wa kamati namba 9, kutoka kundi la 201 ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la filamu nchini(TAFF) Ndg. Paulynus Mtendah akitoa mchango wake kuhusu masuala ya sanaa katika kamati yake walipokutana na wasanii wa tasnia mbalimbali
 • kakaMjumbe wa kamati namb 9 katika Bunge Maalum ambaye pia ni Naibu waziri wa Vijana utamaduni na michezo, Mhe. Juma Nkamia akiongea na Wasania kupitia kamati yake kuhusu masuala ya sanaa na namna wanavyoyapa kipaumbele na kuwahakikishia kwamba Serikali inathamini na itaendelea kuthamini mchongo wa sanaa nchini.
 • kakaMjumbe wa kamati namba 9, kundi la 201 kutoka Zanzibar Mhe. Haidar Madeweyya akimpa mkono Mwanamziki Stara Thomas kama inshara ya kupendezwa na burudani aliyotoa Msanii huyo alipo ombwa kuimba wimbo wake wowote na wanakamati. Aliyeongozana naye ni Mhe. Juma Nkamia, meza kuu ni makamu Mwenyekiti Mhe. William Ngeleja na Mwenyekiti Mhe. Kidawa Salehe haonekani kwenye picha.
 • kakaMjumbe wa kamati namba 9, Mhe. Dkt. Cyril Chami, akichangia katika kamati hiyo, Mhe. Chami kama wajumbe wengine katika kamati amekuwa na mchango mkubwa sana kwa mawazo mbalimbali katika hatua hii ya kutunga katiba ya nchi kwa miaka 50 ijayo.
 • kakaKatika picha ya pamoja ni baadhi ya wajumbe wa kamati namba 9, wakiwa na nyuso za furaha baada ya kumaliza kazi ya kujadili Rasimu ya Pili ya katiba ndani ya muda uliopangwa. Walioketi ni Mwenyekiti Mhe. Kidawa Saleh, makamu Mwenyekiti Mhe. William Ngeleja, kushoto kwa Mwenyekiti ni Mhe. Capt. John Chiligati (Mnadhimi wa kamati bara), Mhe. Mahmoud Mussa (Mnadhimi wa kamati Visiwani), Mhe. Haidar Madeweyya na Katibu wa Kamati ndg. Haji, kutoka kwa makamu mwenyekiti ni Mhe. Mary Makondo na Mhe. Mbaraka Igangu
 • kakaKatika picha ya pamoja ni watendaji wa kamati namba 9 ndg. Asia, Haji, Agnes, Mtumwa, Sudah, Dadi na Said wakiwa na nyuso za furaha, na viongozi wa kamati hiyo Mwenyekiti, Mhe. Saleh Kidawa, makamu Mwenyekiti William Ngeleja, Mhe. Capt. John Chiligati (Mnadhimi wa kamati bara), Dkt. Cyril Chami na Mhe. Mahmoud Mussa (Mnadhimi wa kamati Visiwani).
 • kakaKatika picha ya pamoja ni watendaji wa kamati namba 9 ndg. Asia, Haji, Agnes, Mtumwa, Sudah, Dadi na Said wakiwa na nyuso za furaha baada ya kumaliza kazi nzito ya kuwezesha kamati kukamilisha majukumu waliyokuwa nayo ya kujadili Rasimu ya Katiba ndani ya Kamati.

Habari Mpya

Tarehe : 2014-09-02

Kamati zahitimisha hatua ya kujadili Rasimu katika kila kamati, Septemba 2014

Katika picha ya pamoja ni baadhi ya wajumbe wa kamati namba 9, wakiwa na nyuso za furaha baada ya kumaliza kazi ya kujadili Rasimu ya Pili ya katiba ndani y ...

Zaidi

Tarehe : 2014-09-02

Kamati zahitimisha hatua ya kujadili Rasimu katika kila kamati, Septemba 2014.

Katika picha ya pamoja ni watendaji wa kamati namba 9 ndg. Asia, Haji, Agnes, Mtumwa, Sudah, Dadi na Said wakiwa na nyuso za furaha baada ya kumaliza kazi nzito ya kuwezesha kamati ku ...

Zaidi

Tarehe : 2014-08-25

Wasinii wa tasnia Mbalimbali watemblea Bunge Maalum na kukutana na viongozi mbalimbali Agosti, 2014

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu Mhe. Samuel John Sitta na Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Samia Suluhu wakipokea nyaraka iliyoandaliwa na wasanii wa sanaa mbalimbali, anayewasilisha kwako kwa ...

Zaidi